Monday, August 22, 2011

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAMATI YA SIASA ,TAWI-CCM MOSCOW :21/8/2011, MOSCOW -URUSI

Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya tawi la CCM Moscow-URUSI imemaliza kikao chake cha siku moja, jioni ya tarehe 21/08/2011 mjini Moscow chini ya Uenyekiti wa Kaimu Katibu wa Tawi, Ndg  Bakunda C.D. Pamoja na mambo mengine Kamati ya siasa ya tawi  imeamua yafuatayo;

1. Kamati ya siasa ya tawi imepokea  taarifa ya kiutendaji ya tawi kwa mwaka wa 2010/11 iliyowasilishwa na  Katibu wa halmashauri kuu, itikadi na Uenezi wa Tawi Ndg KOLOWA.K.M na  kupitisha kalenda ya vikao vyote vya tawi kwa mwaka 20111/12 ambapo kalenda  hiyo inaanza kutekelezwa 1/9/2011. Aidha Kamati ya siasa ya tawi inatoa wito kwa WAJUMBE wa Vikao vyote vya tawi na vya Jumuiya, wana CCM, wapenzi na wakereketwa wa hapa URUSI kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha kalenda iliyopitishwa inazingatiwa.Taarifa za Kiutendaji ya tawi inapatikana kupitia website ya tawi ccmmoscow.blogspot.com. au katika facebook   “chama cha mapinduzi-ccm”
2 Kamati ya siasa imepokea na kuridhia taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa katibu wa fedha na uchumi wa Jumuiya ya Vijana ya tawi na Mjumbe wa kamati ya maadili ya Tawi akiwakilisha Jumuiya ya Vijana,Bi Maria Semeni Festo. Aidha Kamati ya Siasa imempongeza kwa uamuzi huo uliozingatia maslahi mapana ya chama chake na Tawi kwa Ujumla. 
3. Aidha Kamati Kuu imejadili masuala mengine ya kijamii na kuwataka watanzania kudumisha Nidhamu zao huku Ugenini na kujikita ktka kuitangaza Tanzania katika nyanja mbalimbali (michezo, utamaduni,na Kuzingati ELIMU). Aidha Kamati ya Siasa  ya tawi inachukua fursa hii kumpongeza Barozi wa Tanzania nchini Urusi Kepten Mstaafu JAKA MWAMBI ,na watendaji wote wa Ubalozi, pamoja na mambo mengine,  kwa juhudi zao za kuwasaidia watanzania hapa urusi na Kuimarisha mkakati wa kuitangaza  Tanzania kupitia Maonyesho ya Utamaduni wa mwafrika yaliofanyika hivi karibuni jijini Moscow pamoja na majukumu mengine walionayo kwa taifa katika eneo lao la Uwakilishi.
 4. Kamati ya Siasa ya Tawi imejadili kwa kina Vipaombele vya Tawi kwa mwaka 2011/12 na  kupitisha kwa kauli moja,kama ifuatavyo :
(a)Uboreshaji wa Mfuko wa tawi kupitia njia mbadala za Ukusanyaji wa vyanzo vya uchumi kupitia jumuiya za tawi
(b)Uzingatiwaji wa Ukusanyaji wa ada za uanachama kupitia kila Jumuiya za tawi na utoaji wa Risiti kwa kila mwanachama hai kwa mwaka 2011/12
(c) Mpango mkakati wa kuongeza wanachama wa tawi na ufunguzi wa SHINA jipya la  watanzania wana-CCM ktk  Mji wa TURA-URUSI. Ufunguzi wa shina hilo jipya unatarajia  kufanyika October.
(d). Jitihada Endelevu za kuwa na MLEZI wa Tawi la CCM Moscow . Kamati ya Siasa ya tawi imemteua aliyekuwa katibu wa Tawi Ndg Boniphace Thomas Assenga kuwa Kiongozi wa JOPO la wajumbe watakaosimamia mchakato wa mawasiliano na  Mlezi wa Tawi CCM MOSCOW na Sekretariet ya CCM ,huko Dar es salaam -Tanzania.
(e) Kuimarishwa kwa jitihada za kimawsiliano na matawi mengine ya CCM yalio nje ya Tanzania ktk lengo la kufahamiana na kubadilishana uzoefu kiutendaji, Matawi hayo ni UK, USA na ITALY.
(f) Maandalizi ya Mpango Mkakati wa Tawi katika kusheherekea Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara
5. Kamati ya siasa ya tawi imeipongeza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Tawi kwa kazi nzuri  na kuitaka iongeze kasi katika utekelezaji wa majukumu yake, ili kuhakikisha mageuzi yaliyokusudiwa yanatekelezwa kwa wakati.
6. Kuhusu suala la maadili ndani ya tawi, Kwa kuzingatia taarifa fupi iliyowasilishwa na  Mjumbe wa Kamati ya Maadili ya tawi  Ndg Manda Iddy Shaaban “Tawi kwa kufuata maagizo ya Chama litaendelea kusimamia maadili, na kuwataka wale waliotakiwa kujipima na kuwajibika watumie muda huo, kujipima na kuwajibika kwa masilahi mapana ya chama na tawi.”
Kamati ya siasa ya tawi imeipa kamati ya maadili muda wa wiki mbili zaidi  iwe imekamilisha report  ya jukumu iliyopewa na  kuwakilisha mapendekezo yake katika kikao kitakachofuata.
Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Tawi inatarajiwa kukutana wakati wowote kipindi cha mwezi Septemba-December 2011 kulingana na agizo la kalenda ya Vikao vya tawi, ambapo pamoja na mambo mengine itatathimini utekelezaji wa maamuzi yake.                                                                              
                  Imetolewa na kuthibitishwa;                   
KOLOWA. K. M.
KATIBU WA NEC, ITIKADI NA UENEZI
TAWI CCM MOSCOW-URUSI


Sunday, August 21, 2011

TAARIFA YA SEKRETARIETI KUU TAWI LA CCM-MOSCOW MWAKA 2010/2011

Ifuatayo ni taarifa ya sekretarieti kuu ya tawi la ccm-moscow URUSI.Taarifa hii ina vipengele vifuatavyo:-

UTANGULIZI
Kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kunipa nafasi hii kutoa taarifa ya utekelezaji na mwelekeo wa chama cha mapinduzi katika tawi letu  hili hapa MOSCOW URUSI katika kikao hiki halali kwa mujibu wa kanuni za chama chetu CCM.
Ndugu wajumbe, kamati ya siasa ya tawi ambayo inahusisha wajumbe 12 tuliopo katika kikao hiki leo napenda kutoa taarifa hii mbele yenu ikiwa na ishara ya wazi kuwa demokrasia katika tawi letu na hata katika jumuiya zetu zilizopo katika  tawi la ccm MOSCOW imekomaa vizuri na inaendelea kukuzwa na mijadala mbalimbali katika mikutano endelevu ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa ujumla.

Ndugu wajumbe: Chama cha mapinduzi tangu kimeanzishwa hapa Moscow urusi kilikuwa na mikakati mbalimbali ya kichama ili kuweza kuhakikisha kuwa tawi linakuwa imara na hatimaye kuzidi kuimarisha chama kwa ujumla.vilevile napenda kusema kutokana na sera na itikadi za chama cha mapinduzi kwa kufuata katiba ya chama na taratibu tulizojiwekea katika chama ni msingi pekee tunajivunia kama chama cha mapinduzi  katika kulinda na kutetea haki na maslahi ya chama kitaifa kwa pamoja.Mbali na jukumu hilo pia ni wajibu wa chama kusaidia wananchi kuelewa serikali yao kuwa inafanya kitu gani  katika kuleta maendeleo ya taifa na hatimaye kuweza kupambana na adui mkubwa wa maendeleo katika nchi yetu ambae ni umaskini.

MAFANIKIO
Ndugu wajumbe wa kamati ya sias:,  kiutendaji na katika kutekeleza majukumu ya chama cha mapinduzi katika tawi letu kumekuwa na mafanikio mbalimbali na makubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa tawi la chama cha mapinduzi Moscow.Haya yote ni katika kutekeleza majukumu ya chama cha mapinduzi tangu kilipoanzishwa.

A.KUPATIKANA KWA WANACHAMA WAPYA.
Chama cha mapinduzi tawi la mocsow limeweza kupata  idadi ya wanachama wapya kwa idadi ya kuridhisha sana kutokana na matokeo mazuri ya wanachama hao kuhamasishwa kwa kiasi cha kutosha na kupelekea kuijiunga na  chama cha mapinduzi tawi(CCM-MOSCOW) hii ikimaanisha kwamba nyongeza hiyo ya wanachama imepelekea tawi kuwa na idadi ya wanachama 97 kwa kipindi cha mwaka 2010/11.Vile vile jumuiya mbalimbali za ccm tawi Moscow zimeweza kuhamasisha na kuwa na idadi kubwa ya wanachama katika jumuiya hizo.Hivyo basi napenda kutoa pongezi kwa jumuiya zote mbili kwa kazi nzuri waliofanya na wanayoifanya mpaka sasa kuhakikisha chama kinakuwa na wanachama wengi kuanzia ngazi ya tawi mpaka kwenye jumuiya zake.Napenda kusema kuwa mafanikio haya hayakupatikana hivi hivi bali  kutokana na shughuli mbalimbali tulizoweza kuzifanya kupitia tawi na jumuiya zake kwa ujumla.Kwa mfano sherehe mbalimbali zilizofanyika kwa kipindi tofauti tofauti za kichama na jumuiya zimeweza kuhamasisha watu wengi kujiunga kutokana kazi nzuri tunayoifanya katika tawi.Hivyo basi napenda kutoa ombi kupitia tawi zoezi hili tunalolitumia mara kwa mara la sherehe katika kuhamasisha watu liwe endelevu,ingawa naamini kuwa uhamasishaji wa mtu mmoja mmoja  upo lakini sio wa kutosha sana ikilinganishwa na sherehe.

B.MAWASILIANO KATIKA TAWI.
Ndugu wajumbe wa kamati ya siasa: chama cha mapinduzi tawi la MOSCOW-URUSI limeweza kuimarisha mawasiliano mazuri kwa ukaribu zaidi kupitia uongozi wa tawi na jumuiya zake  hivyo kupelekea tawi kujulikana  zaidi kitaifa na kimataifa katika matawi mengine yaliyopo ndani na nje ya nchi ya Tanzania.Kwa kipengele hiki cha mawasiliiano napenda kutoa pongeza kwa mwenyekiti wa tawi  Dr.Kamuzora kwa kazi nzuri anayoifanya katika kuhakikisha chama cha mapinduzi tawi la MOSCOW-URUSI linafahamika zaidi kutokana na safari mbalimbali anazozifanya akiwa nyumbani Tanzania na kuweza kupita katika ofisi mbalimbali kitaifa na  kutufikishia ujumbe wa uwepo wa tawi la CCM- Moscow-urusi na hivyo tawi kupewa kipaumbele zaidi.Vilevile pongezi hizi sio tu kwa Dr.kamuzora pia hata kwa viongozi wengine katika chama wanaojituma katika kuhakikisha mawasiliano ya chama katika Nyanja mbalimbali yanapalekea tawi la CCM MOSCOW-URUSI kufahamika zaidi.Kwa mfano jumuiya ya wanawake na jumuiya ya vijana katika tawi zinafahamika sana kutokana na mawasiliano mazuri yaliopo na  yanayoimarishwa  katika jumuiya hizo kupitia viongozi wake na hivyo basi kupelekea chama kufahamika  zaidi pamoja na jumuiya zake ndani na nje ya Tanzania.Hivyo basi napenda kutoa ombi kuwa uimarishwa mzuri wa mawasiliano katika chama na jumuiya uwe wa hali ya juu na upewe  kipaumbele cha kutosha katika kuimarisha tawi letu.

C.MATATIZO.
Pamoja na kuwa na mafanikio katika chama cha CCM MOSCOW-URUSI,pia na  jumuiya zake kimekuwa kinakabiliwa na matatizo mbalimbali na hivyo kuchangia kurudisha nyuma maendeleo ya tawi letu katika utekelezaji wa dhamira na malengo mbalimbali ya chama katika tawi.Matatizo hayo ni kama ifuatavyo:-
1.MIGOGORO.
Ndugu wajumbe wa kamati ya siasa,chama cha mapinduzi katika tawi kimekuwa kinakabiliwa na migogoro mingi sana ya mara kwa mara katika nyadhifa za viongozi wa juu wa tawi na kusababisha kuondoa matumaini kwa wanachama tunaowaongoza na viongozi wengine kwa ujumla.Hali hii imesababisha watu wengi kutopenda kujiunga na chama kutokana na migogoro ambayo iko wazi na ambayo ilikuwa ikiendelea mara kwa mara ndani ya chama katika tawi.

 2.NIDHAMU NA MAADILI.
 Ndugu wajumbe wa kamati ya siasa,nidhamu na maadili katika chama imeshuka kwa kias kikubwa sana.Hali hii imechangiwa sana  kwa viongozi na  wanachama  kutokuheshimiana    viongozi kwa viongozi kutokuheshimiana na hivyo kusababisha nidhamu na maadili katika chama.Kutokana na kushuka huku kwa nidamu na maadili katika chama imesababisha kuondoa matumaini na uaminifu wa wanachama kwa viongozi na vilevile kuondoa uaminifu wa kiongozi katika utendaji wake katika chama.Katika kipengele hiki cha nidamu na maadili natoa ombi kwa viongozi wote kuwa nidhamu na maadili lazima vipewe kipaumbele kwa viongozi wote na wanachama kwa ujumla ili kuweza kuimarisha tawi.Vile vile napenda kuipa nafasi kamati ya nidhamu  na maadili kuchukua hatua zake kikamilifu katika katika kuhakikisha nidhamu na maadili kwa viongozi inachukuliwa hatua za haraka pale inapo onekana kuwa kiongozi ameshindwa kuendana na taratibu ambazo chama cha mapinduzi imejiwekea.Kumbuka kamati ya nidhamu na maadili ni mhimili mkubwa sana kwa chama cha mapinduzi hivyo ni chombo pekee kinachohakikisha nidhamu na maadili ya viongozi katika chama inafuatwa na kutekelezwa.

 3.KUSHINDWA KUKAMILISHA MALENGO YA TAWI.
 Ndugu wajumbe wa kamati ya siasa,chama cha mapinduzi tawi la Moscow limeshindwa      kutimiza malengo yake mengi tu ambayo tuliyapanga katika kipindi cha mwaka 2010/11 ikiwa ni pamoja na kushindwa  kufanya sherehe za kuhamasisha watu kujiunga na chama cha mapinduzi Moscow vilevile na kushindwa kufanya ziara ambazo tulitaka kuzifanya kutembelea miji mingine nje ya Moscow katika kuhamasisha na kufungua mashina sehemu hizo.Hii yote imesababishwa na  migogoro iliyokuwepo  katika chama na kupelekea viongozi kukaa vikao kutatua matatizo ya migogoro hiyo na kuacha kufanya shughuli za kimaendeleo katika kuimarisha chama na kutanua tawi katika sehemu nyingine nje ya Moscow.Vilevile chama katika tawi kimeshindwa kuimarisha mfuko wa tawi hivyo kusababisha tawi kutegemea jumuiya katika kuendesha shughuli zake za kichama zaidi.hivyo basi basi natoa pendekezo katika kipindi hiki cha uongozi mwaka 2011/12 naomba chama kijikite katika kuboresha mfuko wa chama na kutimiza malengo yote tutakayojipangia katika kipindi hiki cha uongozi.Hivyo ni jukumu la kila kiongozi na mwanachama katika kuhakikisha malengo yote tutakayoyapanga yanatimia kuanzia ngazi ya tawi na jumuiya zake kwa ujumla.

D.MAPENDEKEZO
Ndugu wajumbe wa kamati ya siasa,chama cha mapinduzi CCM MOSCOW-URUSI kupitia kamati ya sekretarieti kuu inapenda kutoa mapendekezo yake kama ifuatavyo:-
·         Ushikiano wa viongozi na wanachama kwa ujumla uwe wa uakribu zaidi katika tawi na jumuiya pia ili kuweza kufikia malengo tuliojipangia katika tawi.Hili litakuwa changamaoto nzuri sana ambayo itawezesha viongozi kufanya kazi vizuri na kwa ari na ngumu moja.
·         Kuepuka migogoro na migongano katika tawi na jumuiya ambayo sio ya lazima kwa viongozi wake na wanachama.Hili tukiliondoa katika chama basi kila kiongozi atakuwa anafanya kazi kwa ufanisi kutokana na nafasi yake katika tawi au jumuiya.Na vile vile kusabisha wanachama kuamini utendaji wa kiongozi katika chama.
·         Suala la kuwajibika kwa kila kiongozi lazima lipewe kipaumbele ili kuweza kufikia malengo na mataraji tuliyojiwekea kataka tawi.Kiongozi anatakiwa kuwajibika kutokana na nafasi yake alionayo ili kuweza kutambua mchango wake katika nafasi hiyo kwa kuweza kushirikiana na viongozi wenzie.Hii itatuwezesha kufanya utekelezaji wa majukumu mbalimbali tuliyonayo katika nafasi ya tawi na jumuiya kwa ujumla.
·         Suala la nidhamu na maadili kwa viongozi  linahitaji kusimamiwa kwa ukaribu zaidi kwa kupitia kamati ya nidhamu ili kuweza kulifanya tawi letu na chama kwa ujumla kuwa mfano bora wa kuigwa na matawi mengine ndani na nje Tanzania.

E.VIPAUMBELE:
Ndugu wajumbe wa kamati ya siasa,sekretarieti kuu ya chama katika tawi kupitia vikao vyake viwili ilivyofanya na wajumbe wa kamati hiyo kutoka jumuiya mbalimbali imetoa vipaumbele vifuatavyo:-
·         1)Uboreshaji wa mifuko ya  tawi na jumuiya zote  zijikite katika kuinua mifuko hiyo katika nyanja mbalimbali.
·         2)Ada ya uanachama katika tawi na jumuiya pia zipewe kipaumbele katika makusanyo yake.
·         3) Upande wa kutunisha mifuko njia mbadala elekezi za kukuza mifuko hiyo katika tawi na jumuiya.
·         4)Wajumbe wa Vikao vyote vya CCM au jumuiya wanatakiwa kuvaa sare za Chama.
·         5)Ongezeko la wanachama lazima litiliwe kipamumbele.
·         6)Kufanyika uchaguzi wa viongozi wa tawi mwaka 2012 kulingana na kalenda ya chama
·          7)Jitihada  zifanyike katika kupata mlezi wa tawi.
·         8)Jitihada zifanyike ili kuweza kuwasiliana na matawi mengine ya nje ya nchi.
·          9) Mkakati wa tawi wa kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.
 
F. HITIMISHO
Ndugu wajumbe wa kamati ya siasa mwisho napenda kuchukua nafasi hii kwa kutoa shukarani zangu kwa  kuweza kunisikiliza kwa umakini zaidi kuhusu taarifa hii ya sekretarieti ya chama tawi ambayo inatakiwa kupitishwa na halimashauri kuu ili iweze kwenda kwa wanachama kwa ajili ya kutoa mtazamo na dira ya chama cha mapinduzi tawi la Moscow siku ya mkutano mkuu wa wanachama wote.Asanteni sana kwa kunisikiliza kwa makini naamini yale yaliyomo katika taarifa hii na kuweza kuyasikiliza kwa umakini naamini kila kiongozi atayabeba na atayafanyia kazi vya kutosha ili kuweza kukuza demokrasia ya taifa na utawala bora kwa serikali yetu ya Tanzania.
                                                                                                                                                               
                                                                    ASANTENI

                                                               KOLOWA.K.M                                              21/8/2011
                                    KATIBU WA NEC, ITIKADI NA UENEZAJI TAWI
                                                        


Wednesday, August 3, 2011

KIKAO CHA KWANZA CHA SEKRETARIET MPYA: TAWI LA CCM-MOSCOW: JUMAPILI , 7/8/2011

Ndugu Mjumbe:
Kwa mujibu wa kanuni za Chama Cha Mapinduzi na Hadidu za Rejea za Mwongozo wa tawi la CCM Moscow, UNATAKIWA KUHUDHURIA KIKAO CHA SEKRETARIET YA TAWI la CCM MOSCOW ,kitakachofanyika siku ya Jumapili , tarehe 7 /8/2011 saa 16:30 Jioni - SIMBAD CAFE.

DHIMA YA KIKAO:
1
.Mapitio ya Utendaji wa Jumiya zote za Tawi na Uandaaji wa taarifa kwa wanachama kwa mwaka 2010/11 itakayowasilishwa ktka vikao vya juu vya Uongozi wa tawi .

2. Kuandaa Agenda za kikao cha kamati ya siasa ya tawi.

3. Mapitio ya vipaombele vya maendeleo ya tawi kwa mwaka 2011/12.

Wajumbe wafuatao wanatakiwa kufika bila kukosa kwa kuzingatia Muda uliopangwa:.

1.Kaimu Katibu Tawi: Ndg. Chrispin Bakunda
2.Katibu wa itikadi na Uenezi Tawi: Ndg. Kassim Koloa
3.Katibu wa Uchumi na fedha Tawi : Bi Hilda Kifanga.
4. Katibu UVCCM Tawi. Ndg. Octavian Nyalali
5.Katibu wa Uchumi na fedha UVCCM Tawi . Bi. Maria Semen Festo
6.Katibu UWT Tawi: Bi. Proscovia Jaka Mwambi.
7. Katibu wa Uchumi na fedha UWT Tawi : Bi, Ezelina Mwaifunga.

NB. Kwa Maelezo zaidi au maoni, usisite kuwasiliana na Mamlaka ya Utendaji kupitia mtandao wa facebook “chama cha mapinduzi-ccm” au Kwa Email .ccmmoscow@gmail.com . kwa kusoma taarifa za utendaji tembelea blog ya tawi ccmmoscow.blogspot.com


"TUMETHUBUTU ,TUMEWEZA na TUSONGE MBELE":


Imetolewa na
OFISI YA KATIBU WA TAWI :   3/8/2011
TAWI LA CCM MOSCOW , SHIRIKISHO LA URUSI.


Monday, August 1, 2011

TAMKO LA MKUTANO WA KAMATI KUU YA CCM DODOMA:- 1/8/2011

Mwenyekiti wa CCM Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM mjini Dodoma leo asubuhi.Wengine katika picha kutoka kushoto ni wajumbe wa kamati hiyo Rais mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi,Rais Wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume.Wengine katika picha ni katibu mkuu wa CCM Wilson Mkama na makamu wa CCM bara Pius Msekwa



Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imemaliza kikao chake cha siku moja usiku wa tarehe 31/07/2011 mjini Dodoma chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeamua yafuatayo;

1. Imefanya uteuzi wa makatibu ishirini na saba (27) kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika wilaya hizo. (majina na wilaya zao yameambatanishwa). Pamoja na uteuzi huo, Kamati Kuu imetengua uteuzi wa Makatibu wa Wilaya watatu (3) katika kuboresha ufanisi wa kazi katika wilaya hizo.(majina na wilaya zao yameambatanishwa).


2. Kamati Kuu imepokea na kuridhia taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kuwakilisha Mkoa wa Tabora, Ndugu Rostam Aziz. Aidha imempongeza kwa uamuzi huo uliozingatia maslahi mapana ya chama chake.


3. Kamati Kuu imepokea pia taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Ndugu Rostam Aziz na kuagiza chama kupanga ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga itakayozingatia ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu ya uteuzi wa mgombea.
Aidha Kamati Kuu imeagiza shughuli zote za kampeni kutafanywa na CCM Mkoa, Wilaya na ngazi zote za chama wilayani Igunga. CCM Taifa watashiriki kuongeza nguvu. Chama kinatoa wito kwa wana CCM, wapenzi na wakereketwa wa chama chetu kushiriki kwa pamoja kuhakikisha jimbo linabaki kwa CCM.

4. Kamati Kuu haijaridhishwa na kiwango cha bei ya mafuta ya taa nchini kwa kuwa ndio nishati inayotumiwa na wananchi wengi wenye kipato cha chini. Aidha Kamati Kuu haikuridhishwa na maelezo ya kupandishwa kwa bei ya mafuta hayo kwa kisingizo cha kuzuia uchakachuaji wa mafuta mengine. Hivyo basi, Kamati Kuu imeiagiza Serikali kutafuta njia za kushusha bei ya mafuta ya taa na kuvitaka vyombo vya Serikali vinavyohusika na usimamiaji wa ubora wa mafuta, vihakikishe vinatimiza wajibu wake kuzuia kabisa mtindo wa uchakachuaji wa mafuta nchini na si kupandisha bei ya mafuta ya taa kama suluhisho.

5. Kamati Kuu inasikitishwa na tatizo la umeme nchini kwani athari zake kwa uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja ni kubwa. Hivyo basi imeitaka Serikali kutumia muda iliyopewa wa kurekebisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kuja na mpango wa dharura wa kunusuru hali hii na kisha kulimaliza kabisa tatizo la umeme nchini.

6. Aidha Kamati Kuu imejadili masuala mengine kama; migogoro ya ardhi, tatizo la bei ya pamba, tatizo la uuzaji wa mahindi, migogoro migodini, masuala yanayohusu kero za Muungano na kuagiza Serikali kuyashughulikia kwani yanatatulika.


7. Kamati Kuu imeipongeza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa kazi nzuri ya kutekeleza maamuzi ya NEC na kuitaka iongeze kasi katika utekelezaji huo, ili kuhakikisha mageuzi yaliyokusudiwa yanatekelezwa kwa wakati. Aidha imejadili na kupitisha miundo mipya ya Idara ya Itikadi na Uenezi na Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

8. Kuhusu suala la maadili ndani ya Chama, Chama kinaendelea kusimamia maadili, na kuwataka wale waliotakiwa kujipima na kuwajibika watumie muda huo, kujipima na kuwajibika kwa masilahi mapana ya chama.
Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inatarajiwa kukutana wakati wowote mwezi Septemba, ambapo pamoja na mambo mengine itatathimini utekelezaji wa maamuzi yake.
Imetolewa na:-
Nape M. Nnauye (MNEC)
KATIBU WA NEC, ITIKADI NA UENEZI
DODOMA
1/8/2011

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Wednesday, July 27, 2011

TUMETHUBUTU ,TUMEWEZA, na TUNASONGA MBELE.

 Nape Nnauye akiwa anahutubia Mkutano wa hadhara Mbeya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti uwanjani hapo Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa na Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sita,Christopha Ole Sendeka mbunge wa jimbo la Simanjiro pamoja na Dr.Harrison Mwakyembe mbunge na Naibu Waziri wa Ujenzi na Miundombinu walisema kuwa azma yao ya kupambana na mafisaji bado ipo pale pale.
 
’Ndugu zangu Nyoka akijivua gamba ni kweli sumu huongezeka lakini pia ngozi yake huwa nyororo na anaweza kukimbia vizuri na sumu ambayo imeongezeaka CCM ni kuwabaini na kuwaondoa waovu wote ndani ya chama na Serikali kwasababu watendaji wa Serikali ni wauza duka linalomilikiwa na CCM’’ alisema Nape.
 
Aidha, alikemea tabia za wauguzi wanaowatukana akina mama wajawazito wanapoenda kujifungua kwa kuwatamkia maneno ya kejeri, Polisi wanaogeuza matatizo ya wanaopelekwa vituoni kuwa biashara kwao na maofisa watendaji wa Vijiji na kata wanaotaka fedha wakati wa kusaini fomu za dhamana na nyaraka mbalimbali zikiwemo zile za mikopo ya vyuo vikuu.

Kwa upande wake Mbunge Samwel Sitta aliongeza kuwa hawatanyamaza kamwe hadi pale watakapo hakikisha dhana ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Jakaya Kikwete  ya ‘kujivua gamba’ inakamilika kwa wale wote ambao hawako safi ndani ya chama hicho kwa kuachia madaraka waliyonayo ndani ya chama na Serikali kwa manufaa ya chama na wananchi kwa ujumla, huku akisahau kuwa aliwahi kumkejeli Rais Kikwete na kumwambia kuwa anapaswa kuongeza ukali kidogo katika maamuzi yake.

“Wakati tunapiga kelele bungeni kuhusu mafisadi mimi na wenzangu,baadhi ya wenzetu walituchukia sana na kujenga chuki dhidi yetu kiasi cha wengine kutaka kuninyang’anya kadi ya chama lakini nilisimama imara na leo tunayaona matunda” alisema Sita.

Dr. Mwakyembe alisema kuwa wananchi hasa wanachama wa CCM wanapaswa kuwapuuza wale wote wanaosema kuwa Serikali imeshindwa kuchukua maamuzi magumu na kwamba maamuzi magumu yanaweza kufanywa na watu wasiokuwa na hekima wakiwemo vibaka na Majambazi.

‘’Maamuzi magumu yanafanywa hata na vibaka lakini Serikali ya awamu ya Nne inafanya maamuzi Sahihi na makini’’ alisema Dr. Mwakyembe huku akitafsiliwa kuwa ni majibu dhidi ya Mbunge wa Jimbo l Monduli Edwar Lowasa ambaye hivi karibuni amenukuliwa akisema kuwa Serikali iliyopo madarakani inaumwa ugonjwa wa kutochukua maamuzi magumu.
Alisema kuwa, Rais alipoona baadhi ya viongozi wanaenda  kinyume na matakwa ya waasisi wa chama hicho,ndipo alipoamua kuanzisha dhana hii ili kurudisha sura nzima ya CCM ya zamani ambayo ilikuwa ikiwajali wakulima na wafanyakazi masikini,hivyo tuna kila sababu ya kutembea kifua mbele katika kulisimamia hili.

Mkutano huo Ulioanza kwa MAANDAMANO na UMATI MKUBWA ulihudhuriwa pia na Wabunge wa CCM mkoani hapa, Wenyeviti, makatibu na wajumbe wa ngazi zote kutoka matawi na Kata zote pamoja na wilaya  zinazounda mkoa wa Mbeya ambapo jumla ya wanachama  497 wamepokelewa na kurudisha kadi huku wanachama wapya 2689 wakijiunga na chama hicho na wengine 300 kutoka vyuo vikuu vilivyopo mkoani hapa wakijiunga na chama hicho.


Wabunge waikaanga Wizara ya Kilimo

MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (CCM), ameikomalia Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, akiitaka iwatendee haki wakulima wa mahindi kwa kuwaacha wauze nje ya nchi. Akichangia makadirio ya wizara hiyo kwa mwaka 2011/2012, Anne alisema serikali haipaswi kuwazuia wakulima kuuza mazao yao, kwa kuwa nao ni wafanyabiashara ambao wanalenga kunufaika na kazi wanayoifanya. Mbunge huyo alisema serikali haina budi kubeba jukumu la kuwatumikia wananchi kwa kuhakikisha hawafi njaa, lakini iwaache wauze mazao wanayoyatolea jasho jingi shambani ili yawanufaishe. "Bei ya mazao ili imnufaishe mkulima lazima izidi gharama anazotumia lakini serikali haimsaidii kuondokana na maradhi, ujinga na umasikini kama Katiba inavyotaka," alisema. Alisema bila kilimo bora na imara nchi haiwezi kusogea na kutaja vipaumbele vinavyotakiwa kufanikisha mpango huo kuwa pembejeo, mbolea, mbegu bora na bei nzuri ya mazao.

Mbunge wa Nkasi Kusini, Desderius Mipata (CCM), aliiomba serikali ifungue mipaka ili wakulima waendelee kuuza mazao yao. "Hawa watu masikini kweli waacheni wauze mazao tena nje ya nchi. Mnapotubana kuuza mazao yetu mnataka nini? Tafuteni njia nyingine kunusuru maeneo ya njaa. Sikubaliani hata kidogo na ninyi kutufungia mipaka," alisema.

Innocent Kalogeris (Morogoro Kusini-CCM), aliiomba serikali ishughulikie vurugu kati ya wakulima na wafugaji, kwa kuwa zinaweza kusababisha vifo iwapo zitaachwa. Alisema wafugaji ndio kikwazo cha mafanikio ya kilimo na wamekuwa wakirudisha nyuma juhudi za serikali kuufanya mkoa wa Morogoro kuwa ghala la taifa la chakula. Naye Lediana Mng'ong'o (Viti Maalumu-CCM), alihoji wakulima wanaozunguka maeneo ya ziwa Victoria na Nyasa kutowezeshwa na serikali ili waondokane na kilio cha mara kwa mara cha njaa.

Kwa upande wake, mbunge wa Mpanda Vijijini, Moshi Kakoso (CCM), alitaka serikali iwathamini zaidi maofisa ushirika walioko wilayani na kuwataka wakurugenzi watendaji wa halmashauri kuacha kuwafanya kama watendaji wa ziada wasiokuwa na umuhimu. "Wakurugenzi hawawathamini, ukienda huko wanawaweka karibu na choo… pembejeo za ruzuku nazo haziwanufaishi wakulima, zinachakachuliwa na huko kwetu (Mpanda) pembezoni zinakwenda hadi Rwanda na kwingineko," alisema. Anna Abdallah (Viti Maalumu -CCM), alisema mbolea inapatikana kwa njia za magendo kutokana na serikali kuacha kuwasaidia wakulima wa korosho. Mbunge huyo alisema hakuna pembejeo za korosho kwa mikoa yote inayolima zao hilo, jambo linalosababisha mfuko mmoja wa mbolea aina ya sulphur kuuzwa sh. 50,000. "Bodi ya Korosho ilimaliza muda wake tangu mwaka 2005 ni nani anayesimamia suala la korosho?" alihoji.

Alisema kutokana na kumaliza muda wake, amekuwa akisikia wajumbe wa bodi hiyo huitwa kujadili mambo yanayojitokeza, ilhali uhalali wao umepitwa na wakati. Mbunge huyo aliomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akague matumizi ya fedha zinazopelekwa kwa bodi hiyo. Kwa upande wake, Livingstone Lusinde (Mtera -CCM), alihoji kuendelea kutaja kilimo kuwa uti wa mgongo wa taifa wakati watendaji ni tatizo. Alisema watendaji hao wameshindwa kukibadili kilimo katika vitendo na kubaki wakihubiri na kuzungumza mambo ya kwenye makabrasha, ambayo hayana nafasi kwa sasa.

Akizungumzia kilimo, Lusinde alisema wakulima wanafanya kazi katika mazingira magumu, lakini hawana msaada wa maana wa kuwafanya waondokane na kilimo cha jembe la mkono. Mbunge Ally Keissy (Nkasi Kaskazini -CCM), alisema ni ndoto kufikia mafaniko ya kilimo wakati wakulima wanazuiwa kuuza mazao yao nje ya nchi. Alisema wakulima wa Rukwa wameahidi kuwapiga mawe wabunge wa mkoa huo kwa kuwa serikali imewazuia kuuza mahindi yao nje, wakati ambapo imeshindwa kuyanunua yote. Kuhusu vocha za ruzuku kwa wakulima, alisema utaratibu huo umegubikwa na ufisadi na kuufananisha na EPA nyingine kwa madai kuwa, wao kama wabunge wa Rukwa hawazitaki kwa kuwa usimamizi wake ni mbaya.

SOURCE: gazeti la UHURU. Junne 26/7/11


Warioba alonga

WAZIRI Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, amesema umoja wa taifa utalindwa kwa uongozi imara wa kisiasa. Amesema iwapo dira ya uongozi huo ni umoja, utaimarika lakini kama ni kinyume chake, utakuwa hatarini. Alikuwa akizungumza katika mahojiano na televisheni ya ITV, yaliyotangazwa juzi usiku.
Jaji Warioba alisema tangu nchi ipate uhuru mwaka 1961, yamekuwepo mafanikio mengi, miongoni mwa hayo ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa mwaka 1964. Alisema Muungano ni wa wananchi wenyewe na hautegemei orodha ya mambo ya Muungano, ambayo ni masuala ya kiserikali zaidi.
“Huu Muungano unazungumzwa sana, je, hatujaona mafanikio kwa wananchi? Mwananchi hategemei orodha ya mambo ya Muungano,” alisema. Alisema Watanzania wamekuwa wakishirikiana katika masuala mengi na kuzitumia fursa zinazopatikana katika sehemu zote za Muungano, kama biashara na elimu pasipo hata kujua iwapo mambo hayo ni ya Muungano au la. “Muungano huu umefanikiwa kuwaunganisha wananchi, hauoni wakigombana, serikali ndizo zinavutana. Tujiulize, hivi Muungano tunazungumzia wananchi au tunazungumzia serikali,” alihoji Jaji Warioba.
Alisema Muungano unapozungumzwa ulenge maslahi ya wananchi na si ya madaraka. “Tusije tukafikiri hatutakuwa na matatizo ya Muungano lakini dira ya kuyatatua ina muhusishaje mwananchi,” alihoji Jaji Warioba na kuongeza kwamba, penye mafanikio pana matatizo pia.
Alionya kuwa, demokrasia ya vyama vingi iwe chachu ya kupata mawazo mbadala na si chanzo cha kuligawa taifa kwa misingi ya ukabila, dini na rangi. “Tusipoangalia vyama vimekuwa kama makabila, wafuasi wanaanza kubaguana,” alisema na kuongeza kwamba, dalili za hali hiyo zimeanza kuonekana katika misiba ya viongozi wa vyama vya siasa. “Hili linaniogopesha, msiba unaanza kuwa mtaji wa kisiasa. Umoja wa nchi hii ni jambo la kitaifa,” alisema. Alisema viongozi wa zamani walikuwa si wasomi sana kama wa sasa, ambao ni wa ‘doti com’ lakini walihakikisha umoja wa taifa unalindwa kwa kutambua umuhimu wake.

Jaji Warioba alisema tangu nchi ipate uhuru, yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta mbalimbali, ikiwemo ya elimu, hivyo kuwa na wasomi wengi, sekta ya afya imekuwa na vituo vingi, na ujenzi wa barabara. Katika hatua nyingine, Jaji Warioba alisema viongozi wa kisiasa wa kuchaguliwa wanapaswa kuondolewa madarakani na wananchi waliowachagua, na si vyama. “Hawa wanaochaguliwa na wananchi hivi madaraka yao yako kwenye vyama vya siasa au madaraka yako kwa wananchi,” alihoji Jaji Warioba na kufafanua kwamba, kwa vile ni viongozi wa kuchaguliwa, wenye mamlaka ya kuwaondoa madarakani ni wananchi.
Ingawa hakutaja chama, lakini mgogoro unaoendelea kwa sasa ambao unaoana na hoja ya Jaji Warioba ni ule wa madiwani wa CHADEMA katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, dhidi ya viongozi wa juu wa chama hicho. Uongozi wa juu wa chama hicho unawataka madiwani hao kutohudhuria vikao vya baraza la madiwani na wale wenye nyadhifa katika halmashauri hiyo kujiuzulu, la sivyo watafukuzwa katika chama. Madiwani hao wamekataa kutii maelekezo ya viongozi hao, wakisema wamechaguliwa na wananchi, hivyo waachwe wawatumikie kama walivyowaahidi


Saturday, July 23, 2011

KAIMU KATIBU WA TAWI


TAWI  LA CHAMA CHA  MAPINDUZI MOSCOW RUSSIA LINAWATANGAZIA KUWA Bw. BAKUNDA CHRISPINE DOMISIO ATAKAIMU NAFASI YA KATIBU WA TAWI HADI HAPO ITAKAPOTANGAZWA VINGINEVYO. HII NI KUTOKANA NA KUSAFIRI KWA KATIBU WA TAWI Bw. BONIFACE ASSENGA. WOTE MNAOMBWA KUTOA USHIRIKIANO WENU WA DHATI ILI KUWEZA KUENDELEA IMANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

IMETOLEWA NA OFISI YA KATIBU WA TAWI


Saturday, July 9, 2011

MABADILIKO SEKRETARIET YA TAWI LA CCM MOSCOW



TAWI LA CHAMA CHA MAPINDUZI MOSCOW NCHINI URUSI LINAPENDA KUWATANGAZIA KUWA HALMASHAURI KUU YA TAWI ILIYOKUTANA TAREHE 18/06/2011 ILIFANYA MABADILIKO YA SEKRETARIET YA TAWI NA KAMATI YA UTENDAJI KAMAIFUATAVYO;


GONGA HAPA ILI KUPATA ORODHA KAMILI (download here)

JINA
NAFASI
VIKAO
VIKAO2
1
Dr. ALIFRED KAMUZORA
MWENYEKITI WA TAWI
MJUMBE KAMATI YA SIASA NA HALMASHAURI KUU YA TAWI

2
BONIFACE ASSENGA
KATIBU WA TAWI
MJUMBE KAMATI YA SIASA NA HALMASHAURI KUU YA TAWI
MWENYEKITI SEKRETARIET YA TAWI
3
KASSIM KOLOWA
KATIBU WA SIASA NA UENEZI
MJUMBE KAMATI YA SIASA NA HALMASHAURI KUU YA TAWI
MJUMBE SEKRETARIET YA TAWI
4
SALIMU MFUNGAHEMA
KATIBU WA SIASA NA UENEZI
MJUMBE KAMATI YA SIASA NA HALMASHAURI KUU YA TAWI
MJUMBE SEKRETARIET YA TAWI
5
CHRISPINE BAKUNDA
KATIBU WA UCHUMI NA FEDHA
MJUMBE KAMATI YA SIASA NA HALMASHAURI KUU YA TAWI
MJUMBE SEKRETARIET YA TAWI
6
HILDA KIFANGA
MSAIDIZI WA KATIBU WA UCHUMI NA FEEDHA
MJUMBE KAMATI YA SIASA NA HALMASHAURI KUU YA TAWI
MJUMBE SEKRETARIET YA TAWI
7
MBAROUK MAHMUD
MWENYEKITI UVCCM TAWI
MJUMBE KAMATI YA SIASA NA HALMASHAURI KUU YA TAWI

8
REHEMA SIMBA
MWENYEKITI UWT TAWI
MJUMBE KAMATI YA SIASA NA HALMASHAURI KUU YA TAWI

9
Dr. MOHAMED RAFIK BACHOO
MWENYEKITI WAZAZI TAWI
MJUMBE KAMATI YA SIASA NA HALMASHAURI KUU YA TAWI

10
ODILIA KASIGA
MJUMBE KAMATI YA SIASA TAWI
MJUMBE KAMATI YA SIASA NA HALMASHAURI KUU YA TAWI

11
ALI AMEIR HAJI
MJUMBE KAMATI YA SIASA TAWI
MJUMBE KAMATI YA SIASA NA HALMASHAURI KUU YA TAWI

12
MANDA IDD SHAABAN
MJUMBE KAMATI YA SIASA TAWI
MJUMBE KAMATI YA SIASA NA HALMASHAURI KUU YA TAWI

13
AZIZ CHUMA
MJUMBE KAMATI YA SIASA TAWI
MJUMBE KAMATI YA SIASA NA HALMASHAURI KUU YA TAWI

14
OCTAVIAN NYALALI
KATIBU UVCCM TAWI
MJUMBE HALMASHAURI KUU YA TAWI
MJUMBE SEKRETARIET YA TAWI
15
PROSCOVIA MWAMBI
KATIBU UWT TAWI
MJUMBE HALMASHAURI KUU YA TAWI
MJUMBE SEKRETARIET YA TAWI
16
MARIA SEMEN
KATIBU WA FEDHA UVCCM TAWI
MJUMBE HALMASHAURI KUU YA TAWI
MJUMBE SEKRETARIET YA TAWI
17
EZELINA MWAIFUNGA
KATIBU WA FEDHA UWT TAWI
MJUMBE HALMASHAURI KUU YA TAWI
MJUMBE SEKRETARIET YA TAWI
18
NASSORO KAPONTA
MJUMBE TOKA SHINA BL.6
MJUMBE HALMASHAURI KUU YA TAWI

19
PROSPER NYAMANDA
MJUMBE TOKA SHINA BL.9
MJUMBE HALMASHAURI KUU YA TAWI

20
OMARI KAPILIMA
MJUMBE TOKA SHINA BL.10
MJUMBE HALMASHAURI KUU YA TAWI

21
MJUMBE TOKA SHINA BL.1
MJUMBE HALMASHAURI KUU YA TAWI

22
MJUMBE TOKA SHINA BL.2
MJUMBE HALMASHAURI KUU YA TAWI

23
MJUMBE TOKA SHINA BL.5
MJUMBE HALMASHAURI KUU YA TAWI

24
MJUMBE TOKA SHINA BL.7
MJUMBE HALMASHAURI KUU YA TAWI

25
MJUMBE TOKA SHINA BL.8
MJUMBE HALMASHAURI KUU YA TAWI

26

MJUMBE TOKA SHINA BL.11
MJUMBE HALMASHAURI KUU YA TAWI






 
Авторские права 1996 - 2011 Chama Cha Mapinduzi Tawi la Moscow. Haki zote zimehifadhiwa
.
Best Blogger Gadgets